1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa yaifunga kesi liyozua mauaji ya kimbari Rwanda

16 Februari 2022

Mahakama kuu ya Ufaransa imethibitisha kwamba kesi kuhusiana na kudunguliwa ndege ya rais iliyochochea kuanza kwa mauaji ya halaiki ya Rwanda mwaka 1994, itafungwa.

https://p.dw.com/p/476Ul
Kigali | Macron Besuch in Ruanda
Picha: AFP

Hatua hiyo imeweka kikomo mchakato wa kisheria uliodumu kwa miongo miwili.

Mahakama hiyo imeikataa rufaa ya familia za watu waliouwawa katika shambulizi hilo la kombora lililorushiwa ndege aliyokuwemo rais Juvenal Habyarimana mnamo Aprili 6 mwaka 1994.

Walikuwa wamemtaka jaji huyo aupindue uamuzi wa mahakama ya chini wa kuitupilia mbali kesi hiyo dhidi ya watu walio karibu na rais wa sasa Paul Kagame.

soma zaidi: Rwanda yailaumu Ufaransa kushindwa kuzuia mauaji ya Kimbari

Ndege hiyo aina ya falcon 50 ilikuwa imembeba Rais Habyarimana na Rais wa Burundi Cyprien Ntaryamira waliokuwa wametoka kwenye mkutano wa kilele Tanzania ambako walikuwa wanajadili mzozo ulioko kati ya serikali ya Rwanda na aliyekuwa kiongozi wa kundi la Rwandan Patriotic Front, FPR, Paul Kagame

Chanzo: afp