1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa yafunga viwanja 8 vya ndege ikihofia ugaidi

18 Oktoba 2023

Viwanja vinane vya ndege nchini Ufaransa vimekabiliwa na hali ya tahadhari ya usalama na abiria wamehamishwa katika viwanja kadhaa kufuatia taarifa za vitisho vya mashambulizi zilizotumwa kwa njia ya barua pepe.

https://p.dw.com/p/4XhO4
Frankreich Fernsehansprache von Präsident Macron zu Israel und Gaza
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa.Picha: Eliot Blondet/abaca/picture alliance

Hayo ni kwa mujibu wa duru ya polisi katika taarifa kwa shirika la habari la Ufaransa, AFP.

Duru hiyo imesema kuondolewa kwa abira katika viwanja vya Lille, Lyon, Nantes, Nice, Toulouse na Beauvais karibu na mji wa Paris kungewapa fursa mamlaka kuondoa wasiwasi wowote kwamba vitisho hivyo huenda ni halisi.

Soma zaidi: Kitisho cha bomu chafunga shule Ufaransa

Msemaji wa mamlaka ya safari za ndege nchini Ufaransa amethibitisha kuondolewa kwa abiria kutokana na vitisho vya shambulizi la bomu katika viwanja vya Lille, Lyon, Toulouse na Beauvais, lakini hakuweza mara moja kutoa taarifa zaidi za kina.

Safari za ndege zimecheleweshwa katika viwanja vya Lille, Lyon na Toulouse.

Mamalka hiyo imesema hali sasa ni shwari.