Ufaransa kusitisha mazungumzo na Syria kuhusu Lebanon
31 Desemba 2007Matangazo
Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, amesema atasitisha mazungumzo na Syria mpaka serikali ya mjini Damascus ionyeshe iko tayari kuiruhusu Lebanon ichague rais mpya.
Rais Sarkoz ametangaza hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Cairo, Misiri baada ya kukutana na rais wa Misri, Hosni Mubarak.
Maafisa wa serikali ya Lebanon inayoungwa mkono na nchi za magharibi na viongozi wa upinzani wanaoungwa mkono na Syria, wameshindwa kutatua tofauti zao na kumchagua rais mpya, huku nchi za magharibi zikiilaumu Syria kwa kuvuruga juhudi hizo.
Lebanon imekuwa ikikabiliwa na mgogoro wa kisiasa tangu rais Emile Lahoud alipomaliza awamu yake mnamo tarehe 23 mwezi uliopita.