SanaaBurkina Faso
Ufaransa haitakata mahusiano na Mali, Niger, Burkina Faso
15 Septemba 2023Matangazo
Kauli ya waziri Abdul-Malak ameitoa baada ya wadau katika sekta ya burudani na sanaa nchini Ufaransa kukosoa uamuzi wa kupiga marufuku ushirikiano na wasanii kutoka nchi hizo tatu za Afrika.
Abdul-Malak amekiambia kituo cha redio cha RTL kuwa, Ufaransa iko wazi na inakaribisha wasanii kutoka nchi mbalimbali, na kwamba hakuna mabadiliko yoyote ya sera juu ya hilo.
Matamshi ya waziri huyo wa utamaduni wa Ufaransa yanaonekana kuondoa msuguano na muungano wa wasanii SYNDEAC, ambao ulitaka kukutana na Abdul-Malak baada ya wizara yake kutoa agizo la kusitisha ushirikiano na kukatisha usaidizi wa kifedha kwa taasisi za sanaa kutoka Burkina Faso, Mali na Niger.
Muungano wa SYNDEAC uliitaja marufuku hiyo "kama kitu ambacho hakijawahi kutokea."