1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UEFA yaridhishwa na kiwango cha maandalizi ya Euro 2024

12 Julai 2024

Shirikisho la kandanda Ulaya UEFA limesema limeridhishwa na jinsi mashindano ya Ulaya ya Euro 2024 yalivyoandaliwa nchini Ujerumani kuelekea fainali ya Jumapili itakayochezwa mjini Berlin, kati ya England na Uhispania.

https://p.dw.com/p/4iEnc
Michuano ya EURO 2024 | Jubel | Uhispania vs. Georgia |  Fabian Ruiz
Kiungo wa Uhispania Fabian Ruiz akisherehekea bao lake dhidi ya GeorgiaPicha: Ronald Wittek/EPA

Mkuu wa mashindano wa UEFA Martin Kallen ameliambia shirika la habari la Ujerumani dpa kwamba, wamefurahishwa na idadi ya mashabiki waliofika kwenye michuano hiyo.

Kallen ameeleza kwamba mechi zenyewe zilikuwa nzuri ingawa kulikuwa na matokeo ya kushangaza katika baadhi ya mechi.

Soma pia: Kocha wa Spain asifu uwezo wa kikosi chake Euro 2024

Kallen vile vile ameusifu mfumo wa reli wa Ujerumani ingawa shirika la treni la Ujerumani Deutsche Bahn, limekosolewa pakubwa katika mashindano hayo kutokana na kuchelewa na kufutwa kwa safari nyingi za treni.