1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchunguzi ufanywa kuhusu kifo cha Hariri

21 Februari 2005
https://p.dw.com/p/CFc6

Brussels:

Umoja wa Ulaya leo umekubali kutekeleza mwito wa Marekani wa kutaka uchunguzi wa kimataifa ufanywe kuhusu kuuawa kwa Waziri Mkuu wa zamani wa Lebanon, Rafik al-Hariri. Marehemu ameuawa kwa bomu lililotegeshwa ndani ya gari. Taarifa iliyotolewa mjini Brussels imesema kuwa Baraza la Umoja wa Ulaya linatoa mwito wa kufanywa uchunguzi wa kimataifa haraka kama itakavyowezekana ili mwangaza uweze kupatikana kuhusu wale waliomuua. Umoja wa Ulaya pia unaunga mkono azimio la Umoja wa Mataifa linaloitaka Siria iondoe Wanajeshi wake wote nchini Lebanon. Siria inakanusha tuhuma kuwa inahusika na mauaji ya al-Hariri yaliyotokea juma lililopita.