1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchumi wa mataifa waonesha ishara mzozo wa COVID-19 wapungua

Sekione Kitojo
4 Juni 2020

Kulegezwa zaidi na zaidi hatua za kuwazuwia watu kusalia majumbani mwao na ishara kuwa uchumi wa mataifa mbali mbali unaweza  kuwa umeepuka mzozo mbaya wa janga la virusi vya corona,kumewahamasisha wawekezaji.

https://p.dw.com/p/3dE3h
Hongkong | Alibaba Handelsstart an der Börse in Hongkong
Picha: Getty Images/AFP/Y. Aung Thu

Hata hivyo lakini masoko bado  yanayumba katika kupata  faida pamoja  na  hali  ya wasi  wasi  kuhusiana  na  mvutano  kati ya  China  na Marekani.

Wakati  nchi  zaidi  na  zaidi  taratibu  zinafungua  uchumi  wao uliovurugika  baada  ya  miezi kadhaa  ya  kufungwa  na  kuingizwa kwa  matrilioni  ya  fedha  kama  kichocheo  cha  uchumi  pamoja  na uungaji  mkono  wa   benki  kuu  za  nchi  hizo, masoko  ya  dunia yamekuwa  yakipanda  kwa  wiki  kadhaa  sasa.

Symbolbild -USA- Wirtschaft - Anstieg Dow Jones
Data za biashara katika soko la hisa la mjini New YorkPicha: picture-alliance/W. Ying

Na  katika  ishara  ya  matumaini  kwa  kumbi  za  biashara  za  hisa, masoko  ya  Marekani  yalipanda  kufikia  kiwango  cha juu  kabisa. Wakati  mabaa , mikahawa  na  maeneo  maarufu  ya vivutio  yakianza  tena  kufanyakazi  barani  Ulaya, nchi  kadhaa  ikiwa  ni pamoja  na  Ujerumani, Italia , Austria  na  Ubelgiji  zilianza  kulegeza vizuwizi  vya mipakani, na  kuchochea  matumaini  kwa  ajili  ya sekta  ya  utalii  iliyoathirika  kwa  kiasi  kikubwa wakati  majira  ya joto  yakibisha  hodi.

Ujerumani  pia  itaingiza  euro  bilioni 130  kama kichocheo  cha uchumi  ili kuuanzisha  upya  uchumi huo  mkubwa   katika  bara  la Ulaya, na  baadaye  leo, benki  kuu  ya  Ulaya  inatarajiwa kuimarisha  mpango  wake  wa euro  bilioni 750 wa ununuzi  wa  hati fungani  kwa  kuingiza  euro  za  ziada  bilioni  500.

Deutschland Berlin Pressekonferenz zum Konjunkturpaket | Angela Merkel
Kansela Angela Merkel akizungumza na waandishi habari juu ya kichocheo cha uchumi wa Ujerumani cha euro bilioni 130Picha: Getty Images/AFP/J. MacDougall

Data za ajira

Jana  pia kulishuhudiwa  kutolewa  data nchini  Marekani zinazoonesha  kuwa  nafasi  nyingine  za  ajira  milioni  2.76 zilipotea mwezi  Mei, ambazo  ni  chini  ya  nafasi  za  ajira  milioni 9 zilizokuwa  zikitarajiwa  na  wataalamu  wa  uchumi, ikionesha  kuwa kuna  mwanga unaonekana kwa  mbali.

Katika  biashara mapema  leo, faharasa ya  Hong Kong  iliporomoka kwa  asilimia  0.2, baada  ya  kupanda  kwa  karibu  asilimia  6 katika  muda  wa  kipindi  cha  siku  tatu  zilizopita.

Cathway Pacific Airlines
Shirika la ndege la Hong Kong pia litaruhusiwa kufanyakazi nchini China baada ya kulegezwa vizuwiziPicha: picture-alliance/dpa/J. Favre

Wauzaji walikuwa  wanatupa  jicho  lao  katika  mitaa ya  mji  huo katika  kumbukumbu ya  ukandamizaji  wa  uwanja  wa  Tiananmen, ambao  kwa  kawaida  huvutia  kundi  kubwa  la  watu lakini kumbukumbu  hiyo  imepigwa  marufuku  mwaka  huu  kutokana  na janga  la  virusi  vya  corona.

Pamoja  na  hayo  hali  ya  wasi  wasi   kati  ya  China  na  Marekani inaendelea  kuwapo, na  jana  Washington imeamuru  kusitishwa kwa  safari  zote  za  ndege  za  mashirika  ya  ndege  ya  China kwenda  na  kutoka  Marekani. Lakini China  imesema leo kuwa itaruhusu ndege  za  kigeni ambazo  zimezuiwa  hivi  sasa kufanyakazi  nchini  humo  kuanza  safari za  abiria  kuanzia  Juni 8, na  kuondoa marufuku kwa  ndege  za  Marekani.

Hongkong & Sicherheitsgesetz China | Protest
Waandamanaji mjini Hong KongPicha: picture-alliance/Zuma/Sopa Images/T. Yan

Wakati  huo huo  bunge  la  Hong Kong limepitisha  sheria tata ya mswada wa  wimbo wa taifa leo ambao utafanya  kutoheshimu wimbo wa  taifa  wa  China  kuwa  ni  kosa  la  jinai, hatua  ambayo wakosoaji wanaiona kuwa  ishara  ya  hivi  karibuni  kabisa  ya Beijing  kukaza kamba katika  mji  huo. Uamuzi  huo  unaweza kuzusha  maandamano zaidi katika  mji  huo.