1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchumi wa China waimarika pakubwa

16 Aprili 2021

Pato la jumla la ndani la China limepanda kwa asilimia 18.3 katika robo ya kwanza ya mwaka 2021, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana, hii ikiwa ni kulingana na taarifa rasmi zilizochapishwa.

https://p.dw.com/p/3s7ST
Asien I China I Neujahr I LUNAR
Picha: Ju Peng/Xinhua/picture alliance

Ongezeko hilo ni la juu kabisa tangu China ilipoanza kuweka rekodi za kila robo ya mwaka, mnamo mwaka 1992.

Wakati janga la virusi vya corona likizidi kudhoofisha masoko ya ulimwengu, taifa hilo la pili kwa nguvu ya kiuchumi duniani linaonekana kuanza kurejea katika hali ya kawaida kutoka kwenye mgogoro unaosababishwa na janga hilo, hali iliyochochewa na shughuli za kiviwanda na kiwango cha juu zaidi cha mauzo ya nje, kuliko ilivyotarajiwa.

soma zaidi:Maoni: China yatumia chanjo ya corona kutanuwa ushawishi

Hata hivyo takwimu hizi za karibuni ziko chini ya matarajio. Uchunguzi wa shirika la Reuters wa maoni ya wachumi ulionyesha ukuaji kwa asilimia 19.