1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMsumbiji

Zaidi ya raia milioni 17 wa Msumbiji kumchagua rais mpya

7 Oktoba 2024

Zaidi ya raia milioni 17 wa Msumbiji wanatarajiwa kumpigia kura rais mpya siku ya Jumatano katika uchaguzi ambao haumuhishi rais aliyeko madarakani Filipe Nyusi ambaye anamalizia muhula wake wa pili.

https://p.dw.com/p/4lU0T
Uchaguzi nchini Msumbiji 2024 | Daniel Chapo | Lutero Simango | Ossufo Momade | Venâncio Mondlane
Picha ya pamoja ya wagombea wa urais nchini Msumbiji Picha: ALFREDO ZUNIGA/AFP/Getty Images/Nádia Issufo/DW/Bernardo Jequete/DW/Cristiane Vieira Teixeira/DW

Chama cha Rais Felipe Nyusi cha FRELIMO kimeshika hatamu tangu nchi hiyo ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa ureno mwaka 1975.

Mara hii Daniel Chapo aliyezaliwa baada ya uhuru wa nchi hiyo ndiye atakayekiwakilisha chama cha FRELIMO kuwania urais wa nchi hiyo.

Wagombea wengine ni pamoja na Ossufo Momade, kiongozi wa chama cha RENAMO tangu 2018 ambaye alishindwa katika uchaguzi wa urais wa 2019 kwa Nyusi na Lutero Simango wa chama cha MDM, chama kilichoundwa mwaka 2009 kutokana na mgawanyiko katika chama cha RENAMO.

Raia wa Msumbiji wanatarajia kuwa rais mpya ataleta amani kwenye nchi hiyo maskini lakini yenye utajiri wa mafuta na gesi ambayo imekubwa na msukosuko wa vita vya waasi hasa maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo kwa karibu miaka saba.