1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msumbiji kupiga kura Oktoba 9

1 Oktoba 2024

Wapigakura nchini Msumbiji watashiriki zoezi la uchaguzi wa rais na bunge mnamo tarehe 9 Oktoba na kuufikisha mwisho utawala wa mihula miwili ya Rais Filipe Nyusi.

https://p.dw.com/p/4lHQR
Daniel Chapo FRELIMO
Mgombea urais wa Msumbiji kwa tiketi ya chama tawala cha FRELIMO; Daniel Chappo.Picha: Sitoi Lutxeque/DW

Uchaguzi huo mkuu utafanyika katika wakati serikali inaendelea kukabiliana na makundi ya wapiganaji yanayofungamanishwa na kundi linalojiita Dola la Kiislamu (IS) katika mkoa wenye utajiri wa gesi wa Cabo-Delgado kaskazini mwa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.

Soma zaidi: 

Vikosi vya Tanzania vitaendelea kubaki Msumbiji

Miongoni mwa wagombea urais katika uchaguzi huo ni Daniel Chapo mwenye umri wa miaka 47 aliyewahi kuwa mtangazaji akisimama kwa tiketi ya chama tawala cha Frelimo.

Licha ya kutokuwa na umaarufu mkubwa katika jukwaa la siasa za Msumbiji, anatarajiwa kushinda  kutokana na umaarufu wa chama chake.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW