1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa bunge Malaysia:

21 Machi 2004
https://p.dw.com/p/CFeK
KUALA LUMPUR: Nchini Malaysia watu zaidi ya miliyoni kumi wameitwa kwenda kulichagua bunge jipya hii leo. Kuna uhakika kuwa mwungano wa vyama vya serikali National Front wa Waziri Mkuu Abdullah Ahmad Badawi kwa mara nyingine utanyakua si kasoro ya thuluthi mbili ya viti bungeni. Waangalizi wanangojea kwa hamu kuona matokeo ya chama cha itikadi kali cha Kiislamu PAS katika chaguzi za mabunge ya mikoa kumi na mbili zinazofanyika wakati huo huo na uchaguzi wa bunge. Waislamu hao wa itikadi kali wanaendesha serikali katika mikoa miwili, wakiwa sasa wanatazamia kushinda pia katika mikoa mine mengine.