Uchaguzi wa Bunge la Umoja wa Ulaya
8 Juni 2009Matangazo
BERLIN:
Vyama vinavyotawala katika serikali ya
mseto nchini Ujerumani vya CDU na
CSU vimeongoza katika uchaguzi wa
bunge la Umoja wa Ulaya kwa kupata
asilimia 37. 9 ya kura.
Chama kingine kilichomo katika serikali ya hiyo cha SPD hakikufanya vizuri katika uchaguzi huo na kimepata asilimia 20. 8 ya kura.
Vyama vya upinzani vya FDP,Kijani na cha mrengo wa shoto vimefanikiwa kuongeza idadi ya viti .
Katika mandhari ya Ulaya kwa jumla vyama vya mrengo mkali wa kulia vimepata mafanikio makubwa katika uchaguzi wa bunge la Umoja wa Ulaya.
Nchini Uingereza chama cha kibaguzi BNP kimefanikiwa kupata kiti katika bunge hilo kwa mara ya kwanza.