1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa bunge Burundi.

4 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CExQ

Bujumbura:

Warundi leo wanapiga kura katika uchaguzi wa bunge, ambayo ni hatua nyengine katika utekelezaji wa mpango wa amani ya nchi hiyo, unaolenga kumaliza vita vya miaka 12 vya wenyewe kwa wenyewe. Wachambuzi wanaashiria kwamba chama cha waasi wa zamani CNDD-FDD, kina nafasi kubwa zaidi ya kushinda uchaguzi huo. Jumla ya vyama 25 vinashiriki. Vita vya wenyewe kwa wenyewe baina ya Wahutu walio wengi na Watutsi waliokua wakidhibiti hatamu za uongozi, vimesaababisha vifo vya zaidi ya watu laki tatu.