1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi mkuu kufanyika Januari, 2024 nchini Pakistan

21 Septemba 2023

Uchaguzi mkuu uliyocheleweshwa nchini Pakistan, hatimaye utafanyika mnamo wiki ya mwisho ya mwezi Januari hapo mwakani.

https://p.dw.com/p/4Wf72
Pakistan Shah Mahmood Qureshi
Picha: Anjum Naveed/AP Photo/picture alliance

Hayo yameelezwa na tume huru ya uchaguzi nchini humo, na hivyo kumaliza miezi kadhaa ya uvumi kuhusu kuyumba kwa demokrasia katika taifa hilo la Asia Kusini.

Uvumi huo ulitokana na watu kudhani kuwa jeshi lenye nguvu, ambalo liliitawala Pakistan kwa miongo kadhaa, lilitaka kuendelea na udhibiti wao kupitia utawala wa mpito.

Anwaar-ul-Haq Kakar aapishwa kama waziri mkuu wa mpito wa Pakistan

Kwa mujibu wa katiba ya Pakistan, uchaguzi huo ulitakiwa kufanyika mwezi Novemba baada ya serikali inayomaliza muda wake kuondoka madarakani mwezi agosti ambapo pia kiongozi wa mpito aliteuliwa. 

Marekani, Umoja wa Ulaya na mashirika mengine ya kimataifa wametoa wito wa kuwepo kwa uchaguzi huru na haki utakaosaidia taifa hilo lenye silaha za nyuklia kujikwamua katika mgogoro wa kiuchumi.