1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Uchafuzi wa mazingira wasababisha vifo milioni 9 duniani.

20 Mei 2022

Utafiti mpya unaonesha takribani watu milioni 9 hufa kila mwaka duniani kote kutokana na uchafuzi wa mazingira unaofanywa na maendeleo ya shughuli za kibinadamu ikiwemo viwanda, mataifa yanayoendelea huathirika zaidi.

https://p.dw.com/p/4BTfO
Iran Teheran | Luftverschmutzung
Picha: ATTA KENARE/AFP/Getty Images

Takribani watu milioni tisa hufa kila mwaka duniani kote kutokana na uchafuzi wa mazingira wa kila aina, ikiwemo hewa chafu kutoka kwenye malori, magari na ongezeko la asilimia 55 la viwanda tangu mwaka 2000.

Taarifa hiyo ilitokana  nautafiti wa vifo ulimwenguni na viwango vya uchafuzi wa mazingira iliyochapishwa na jarida la Lancet, linalozungumzia masuala ya afya.

 Kulingana na utafiti huo mpya, Marekani ndiyo nchi pekee iliyoendelea kiviwanda katika mataifa 10 bora, yenye vifo vitokanavyo na uchafuzi wa mazingira, ikishika nafasi ya saba ikiwa na vifo 142,883 kutokana na uchafuzi wa mazingira kwa mwaka 2019, ikiwa kati ya Bagladesh na Ethiopia.

Soma zaidi:Hasara zaongezeka kutokana na majanga ya mabadiliko ya hewa

India na China zinaongoza duniani kwa vifo vitokanavyo na uchafuzi wa mazingira, ikiwa ni takribani vifo milioni 2.4 hadi vifo milioni 2.2 kwa mwaka, ingawa mataifa hayo mawili pia yana idadi kubwa ya watu duniani.

Wataalamu wa afya:Uchafunzi wa mazingira waathiri afya ya binadamu

Mkurugenzi wa Mpango wa Kimataifa wa Afya ya Umma na uchafuzi wa Mazingira katika Chuo cha Boston alisema vifo milioni tisa ni vifo vingi na habari mbaya ni kwamba vifo hivyo havipungui.

WHO: Unene unachangia magonjwa mengi

Kulingana na Dokta Lynn Goldman, mkuu wa Chuo Kikuu cha George Washington kwenye shule kuu ya afya ya umma, ambaye hakuwa sehemu ya utafiti huo anasema vifo hivyo vinaweza kuzuilika.

 Landrigan alifafanua kuwa vyeti vya vifo hivyo havielezi uchafuzi wa mazingira, bali vinaorodhesha magonjwa ya moyo, kiharusi, saratani ya mapafu, magonjwa mengine ya mapafu na kisukari ambayo yanahusiana sana na uchafuzi wa mazingira.

Wataalam watano wa afya ya umma na uchafuzi wa hewa, akiwemo Goldman, waliliambia  shirika la habari la Associated Press kuwa, utafiti huo unazingatia mawazo ya kisayansi.

soma zaidi:China yaonya uhusiano mbaya na Marekani utarudisha nyuma mazungumzo ya hali ya hewa

Dokta Renee Salas, wa chumba cha dharura na Profesa wa Chuo Kikuu cha Harvard ambaye hakuwa sehemu ya utafiti huo, anasema taasisi ya magonjwa ya moyo iliyopo Marekani ilibaini zaidi ya muongo mmoja uliopita kuwa chembe za uchafuzi wa mazingira ikiwemo kuchomwa kwa mabaki na mafuta ni chanzo cha ugonjwa wa moyo na vifo.

Kwa mujibu wa Salas, wakati watu wanapambana kuepuka shinikizo la damu na kupunguza vyakula vyenye mafuta, wachache wanatambua kuwa kudhibiti uchafuzi wa hewa, ni dawa muhimu ya kuimarisha afya ya mioyo yao.

  Vyanzo vya uchafuzi wa hewa

Landrigan anasema robo tatu ya vifo vilitokana na uchafuzi wa hewa na sehemu kubwa ya hiyo ni mchanganyiko wa uchafuzi wa mazingira kutoka kwenye vyanzo kama vile mitambo ya nishati ya makaa ya mawe na viwanda vya chuma, magari, malori na mabasi.

Alisema hilo ni tatizo kubwa duniani na kwamba hali inazidi kuwa mbaya duniani kote kadri nchi zinavyoendelea na miji kukua.

Dan Greenbaum, rais wa Taasisi ya Afya,ambaye hakuwa sehemu ya utafiti huo, anabaishia kuwa vifo vitokanavyo na uchafuzi wa mazingira vinaongezeka kwenye nchi ambazo zina msongamano mkubwa wa watu kama vile barani Asia.

Soma zaidi:Dunia inahitaji hatua thabiti za kulinda mazingira

Aliongeza kwamba, huko fedha na rasilimali za serikali kushughulikia tatizo la uchafuzi wa mazingira ni kidogo na hivyo kushindwa kukabiliana na changamoto nyingine ikiwemo upatikanaji wa huduma za afya na lishe pamoja na uchafuzi wa mazingira.

Landrigan alisema nchini Marekani, watu wapatao 20,000 hufa kila mwaka kutokana na shinikizo la damu linalosababishwa na uchafuzi wa mazingira, magonjwa ya moyo na figo, hasa kutokana na kazi. 

Richard Fuller, mwanzilishi wa shirika lialojihusisha na masuala ya afya na mipango ya kuondokana na uchafuzi wa mazingira, alisema aina za kisasa za uchafuzi wa mazingira zinaongezeka katika nchi nyingi, haswa zile zinazoendelea, lakini zilipungua kutoka mwaka 2000 hadi 2019 nchini Marekani, Umoja wa Ulaya na Ethiopia.

Kiwanda cha kurejeleza taka huko Hawassa,Ethiopia