1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ubelgiji haitopeleka vikosi vyake Mali

16 Februari 2022

Ubelgiji kwa sasa imeondoa uwezekano wa kutuma kikosi cha wanajeshi 250 nchini Mali. Haya yamesemwa na waziri wa ulinzi wa Ubelgiji wakati ambapo vikosi vya Ulaya vinaondoka katika eneo la Sahel.

https://p.dw.com/p/476YH
Mali Bamako Junta-Chef Assimi Goita (R) mit Premier Maïga
Picha: FLORENT VERGNES/AFP

Waziri wa ulinzi Ludivine Dedonder ameiambia kamati ya bunge ya Ubelgiji kwamba hali ya usalama iliyoko sasa haikubali kupeleka wanajeshi.

Mabadiliko ya mpango huo yanakuja wakati ambapo Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anadaiwa kuwa tayari kutangaza kwamba vikosi vya Ufaransa vitaondolewa kutoka Mali na kupelekwa kwengine katika eneo la Sahel, kufuatia kuvunjika kwa mahusiano kati ya jeshi la nchi hiyo.

soma zaidi: Hatma ya vikosi vya Ufaransa Mali mashakani

Duru za kiusalama zinasema tangazo la Macron litatolewa wakati wa mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika mjini Brussels hapo kesho Alhamis na Ijumaa. 

Chanzo: afp