1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ubalozi wa Saudia warejesha shughuli zake Iran

9 Agosti 2023

Ubalozi wa Saudi Arabia nchini Iran umerejesha shughuli zake, kufuatia mataifa hayo kukata mahusiano kwa miaka saba na kusababisha ubalozi huo kufungwa.

https://p.dw.com/p/4UxuT
 Iran Teheran | Prinz Faisal bin Farhan al Saud
Picha: Rouzbeh Fouladi/ZUMA/IMAGO

Iran ambayo ina watu wengi wa madhehebu ya Shia na Saudi Arabia ya WaSunni zimekubaliana kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na kufungua tena balozi zao baada ya kutangaza kufikia makubaliano yaliyoratibiwa na China mwezi Machi, hii ikiwa ni kulingana na shirika rasmi la habari la Iran, IRNA.

Hata hivyo, Riyadh bado haijathibitisha taarifa za kufunguliwa tena kwa ubalozi huo. Mahusiano ya mahasimu hao wa muda mrefu wa kikanda yaliingia doa mwaka 2016 baada ya ujumbe wa kidiplomasia wa Saudi Arabia nchini Iran kushambuliwa wakati wa maandamano ya kupinga uamuzi wa Riyadh wa kumnyonga kiongozi wa kidini wa madhehebu ya Shia, Nimr al-Nimr.

Mwezi Juni, Iran ilifungua upya ubalozi wake mjini Riyadh kwa hafla iliyohusisha kupandisha bendera yake.