1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMyanmar

China yawataka raia wake kuondoka mpakani mwa Myanmar

Hawa Bihoga
28 Desemba 2023

Ubalozi wa China nchini Myanmar umewataka raia wake kuondoka katika wilaya ya kaskazini ilio katika mpaka wa pamoja wa nchi hizo mbili.

https://p.dw.com/p/4aebb
Myanmar | Rais wakikimbia mapigano jimbo la Kayah
Raia walionaswa katikati ya mashambulizi ya anga katika jimbo la Kayah, Myanmar.Picha: Stringer/File Photo/REUTERS

Wito huo umetokana na kile Beijing ilichokitaja kuwa hatari ya usalama wakati makundi ya uasi wa makabila ya wachache yakipambana na utawala wa kijeshi.

Waasi hao wameteka miji kadhaa na vituo muhimu vya mpakani venye umuhimu wa kibiashara na China, katika kile ambacho wachambuzi wanasema ndiyo changamoto kubwa zaidi ya kijeshi kwa utawala wa kijeshi tangu uliponyakua madaraka mwaka 2021.

Mapema mwezi huu Beijing ilisema iliratibu mazungumzo ya upatanishi kati ya jeshi na makundi matatu ya uasi na kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda.

Hata hivyo makabiliano yameendelea katika baadhi ya maeneo ya jimbo la Shan, huku kundi mojawapo la waasi la Jeshi la Ukombozi la Ta'ang, TNLA, likidadi kuteka miji mwili zaidi katika siku za karibuni.