1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tusk aanza uwaziri mkuu wa Poland kwa mara nyengine

13 Desemba 2023

Waziri mkuu mpya wa Poland, Donald Tusk, amesema serikali yake itapigania mataifa ya Magharibi yaendelee kuisaidia Ukraine, huku akiahidi kuwa Warsaw itakuwa mwanachama imara wa muungano wa kijeshi wa NATO.

https://p.dw.com/p/4a5nv
Waziri Mkuu mpya wa Poland, Donald Tusk.
Waziri Mkuu mpya wa Poland, Donald Tusk.Picha: Aleksandra Szmigiel/REUTERS

Bunge lilipiga kura ya kuwa na imani na serikali ya Tusk siku ya Jumanne (Disemba 12), ambapo kwenye hotuba yake ya ufunguzi, kiongozi huyo alitowa wito wa mshikamano baina ya pande hasimu za kisiasa nchini humo.

Tusk, anayefuata siasa za mrengo wa kati, aliwahi kuwa waziri mkuu wa Poland kutoka mwaka 2007 hadi 2014, alipochaguliwa kuwa rais wa Baraza la Ulaya, nafasi aliyoishikilia hadi mwaka 2019.

Soma zaidi: Wabunge wa Poland wanajiandaa kuipigia kura serikali ya Tusk

Sasa amerudi madarakani akiongoza muungano wa vyama vya siasa vilivyoshinda uchaguzi wa Oktoba mwaka huu, kwa ahadi za kuirejesha Poland kwenye majukwaa ya kimataifa.