1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Uturuki limefanya mashambulizi ya anga Iraq

4 Oktoba 2023

Wizara ya Ulinzi ya Uturuki imesema jeshi lake la anga limevurumisha makombora huko mashariki mwa Iraq na kuteketetezha maeneo lengwa 16 ya wapiganaji wa chama cha wafanyakazi cha Wakurdi PKK.

https://p.dw.com/p/4X5Af
Wanajeshi wa Uturuki wakiwa katika kambi yao katikati ya milima ya Ikiyaka na Daglica, karibu na mpaka wa Iraq wa Hakkari
Wanajeshi wa Uturuki wakiwa katika kambi yao katikati ya milima ya Ikiyaka na Daglica, karibu na mpaka wa Iraq wa HakkariPicha: Ozkan Bilgin/AA/picture alliance

Wizara ya ulinzi ya Uturuki imesema operesheni hiyo imefanyika katika maeneo ya Metina, Gara, Hakurk, Qandil na Asos na kwamba ilifanyika kwa uangalifu kuwalinda raia.

Hatua hiyo ni baada ya Jumapili washambuliaji wawili waliojitoa muhanga kujiripua katika majengo ya serikali huko Ankara na kusababisha watu wote walikuwamo kupoteza maisha na polisi wawili kujeruhiwa, shambulizi ambalo PKK ilidai imehusika.