1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Itakuwa ni mechi ya kukata na shoka

Deo Kaji Makomba
6 Agosti 2020

Mlinzi wa klabu ya soka ya Manchester City ya Uingereza Aymeric Laporte amesema kuwa wako tayari kupambana na Real Madrid Ijumaa

https://p.dw.com/p/3gX9L
Fussballer Aymeric Laporte
Aymeric LaportePicha: Getty Images/AFP/M. Bureau

Mlinzi wa klabu ya soka ya Manchester City ya Uingereza Aymeric Laporte amesema kuwa wako tayari kupambana na Real Madrid Ijumaa kwa ajili ya kuendeleza harakati za klabu yake kutaka kutwaa taji la ligi ya mabingwa kwa mara ya kwanza.

Mabingwa hao mara sita wa Uingereza waliongoza 2-1 katika mkondo wa kwanza  baada ya adhabu ya  Kevin de Bruyne katika eneo la penaiti kuwa salama  kuelekea karibu na ushindi huko Bernabeu.

Ushindi huo ulipatikana mnamo mwezi Februari kabla ya mlipuko wa virus vya Corona kusitisha mchezo wa mpira wa miguu.

Laporte, ambaye alipata jeraha katika mechi ya duru ya kwanza, anatarajia mapumziko ya miezi mitano hayatapelekea sababu kubwa ya kuamua nani atalekea Lisbon kwa mechi za robo fainali, ambapo pale mashindano madogo ya ligi ya mabingwa yatafanyika.

"Sijui ni jinsi gani kati ya mipangilio itaathiri mchezo," alisema.

"Lakini tuko tayari kucheza dhidi yao na tutakuwa tayari kupigana hadi mwisho.

"Natumaini tunaweza kushinda na kuendelea na hatua inayofuata."

City wamefika robo fainali katika misimu miwili iliyopita lakini iliyotolewa na vilabu vyenzake vya Kiingereza Tottenham Hotspur mwaka jana na Liverpool msimu uliopita.

Wageni Madrid wako katika hali nzuri mbele ya safari yao ya Etihad ya City Uwanja uliokuwa umebeba ushindani wa michezo 10 wakati City wamepoteza mbili kati ya 10 yao ya mwisho ikiwa ni pamoja na nusu fainali ya Kombe la FA kwa Arsenal.

"Real Madrid wana wachezaji wengi wa kiwangocha juu na mzunguko wa pili utaenda kuwa ngumu sana kwa timu zote mbili, "alisema mshambuliaji wa City, Gabriel Jesus.

"Chochote kinaweza kutokea. Nyumbani tunaweza kudhibiti mchezo, lakini lazima ujue wanaweza kutupiga. "

Chanzo: DPA