1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Scholz awasili Magdeburg, idadi ya vifo yaongezeka

21 Desemba 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ameutembelea mji wa Magdeburg siku ya Jumamosi, saa kadhaa baada ya mwanaume mmoja kuvurumisha gari kwenye soko la Krismasi. Idadi ya vifo imefikia watu watano.

https://p.dw.com/p/4oRjw
Magdeburg 2024 | Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akiutembelea mji wa Magdeburg
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akiutembelea mji wa Magdeburg: 21.12.2024Picha: Ebrahim Noroozi/AP Photo/picture alliance

Alipoutembelea mji huo wa katikati mwa Ujerumani wa Magdeburg, Kansela Olaf Scholz amelaani shambulio hilo aliloliita kuwa baya katika soko la Krismasi lililosababisha vifo vya watu watano na kuwajeruhi wengine karibu 200.

Scholz amesema: "Hakuna mahali pa amani na furaha zaidi kuliko soko la Krismasi. Ni kitendo cha kutisha kuwadhuru na kuua watu wengi kwa ukatili katika eneo kama hili."

Polisi inasema tukio hilo limefanywa na mshukiwa mwenye umri wa miaka 50, ambaye alihamia Ujerumani akitokea Saudi Arabia.

Inaarifiwa mwanaume huyo  anayefanya kazi ya udaktari alilielekeza kwa makusudi gari alilolikodi kwenye umati mkubwa wa watu uliokuwa umekusanyika kwenye soko la Krismasi la Magdeburg.

Mshukiwa huyo alikamatwa baadae na bado yumo kwenye mikono ya vyombo vya dola na taarifa za awali zinasema huenda alifanya shambulizi hilo peke yake.

Rambirambi zaeendelea kumiminika kutoka kwa viongozi mbalimbali duniani 

Rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen
Rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der LeyenPicha: Eitan Abramovich/AFP

Rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen ametuma salamu za pole kwa wahanga wa shambulizi, baada ya gari kuvamia soko la Krisimas kwenye mji wa Magdeburg Ijumaa usiku.

Von der Leyen ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X akisema yuko pamoja na jamaa na marafiki wa wahanga wa shambulizi hilo huku akiwashukuru polisi na watoa huduma za uokozi. 

Karibu watu wawili wamekufa, ikiwa ni pamoja na mtoto mdogo pamoja na wengine 60 wamejeruhiwa, baada ya dereva kuliingiza gari kwenye soko hilo.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kujihami, NATO Mark Rutte naye ametuma salamu za pole kwa kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akieleza kusimama pamoja na wahanga pamoja na familia zao.

Polisi inamshikilia mtuhumiwa, raia wa Saudi Arabia, ambaye ni daktari wa binaadamu anayeishi jimbo la Saxony-Anhalt kwa shambulizi hilo.

Ibada ya kumbukumbu ya tukio hilo kufanyika Magdeburg

Tamara Zieschang, waziri wa mambo ya ndani wa jimbo la Saxony-Anhalt, alisema mshukiwa huyo anaishi Ujerumani tangu 2006 na ana ukaazi wa kudumu.

Soma pia:Maoni: Mashambulizi ya Berlin yataibadilisha Ujerumani

Ujerumani | gari lavamia soko la Krismas Magdeburg
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Saxony-Anhalt Tamara Zieschang, Waziri Mkuu wa Jimbo la Saxony-Anhalt Reiner Haseloff na meya wa Magdeburg Simone Borris wakizungumza na wanahabari baada ya gari kugonga umati wa watu kwenye soko la Krismasi na kuwajeruhi zaidi ya watu 60, mnamo Desemba 20, 2024.Picha: JOHN MACDOUGALL/AFP

Kunatarajiwa kufanyika ibada kufuatia shambulizi hilo hii leo Jumamosi majira ya saa moja za usiku katika kanisa kuu la Magdeburg.

Waziri wa Mambo ya Ndani Nancy Faeser na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz pia wanatarajiwa kufika kwenye eneo hilo leo Jumamosi. Scholz aliandika kwenye mtandao wa X "Fikra zangu ziko na waathiriwa na familia zao. Tunasimama pamoja na watu wa Magdeburg." "Shukrani zangu ziwafikie jeshi la uokozi waliojitolea kwa hali na mali katika masaa yaliyojaa mashaka makubwa."

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric alisema Umoja wa Mataifa ulishangazwa na taarifa za tukio hilo.

"Tunatuma rambirambi zetu kwa familia za waathiriwa, vile vile kwa serikali na watu wa Shirikisho la Ujerumani. Tunatamani
waliojeruhiwa wapate ahueni ya haraka," alisema katika taarifa.

Soma pia:Shambulizi mjini Berlin: Dunia yatoa rambirambi

Rambirambi zimemiminika kutoka kwa viongozi wengine, ambao ni pamoja na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer na Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg ambao wote walisema wameshtushwa na tukio hilo.

Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya Ursula von der Leyen
Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya Ursula von der Leyen amekosoa vikali shambulizi, baada ya gari kuvamia soko la Krismas katika mji wa Magdeburg mashariki mwa UjerumaniPicha: Johanna Geron/REUTERS

Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya Ursula von der Leyen alisema "fikra zangu ziko pamoja na waathiriwa" baada ya shambulizi la "katili na la kipuuzi", katika chapisho lake kwenye X.

Viongozi wakosoa shambulizi hilo 

Von der Leyen, mwanasiasa wa kihafidhina wa Ujerumani ambaye anaongoza chombo kikuu tendaji kwenye Umoja wa Ulaya, alitoa wito kwa "kitendo cha vurugu" "kuchunguzwa na adhabu kali kutolewa."

soma pia:Scholz aunga mkono kufukuzwa wahalifu wa Syria, Afghanistan

Saudi Arabia nayo ilionyesha "mshikamano" na Ujerumani kufuatia kisa hicho kilichomuhusisha raia wake. "tuko pamoja na watu wa Ujerumani na familia za waathiriwa", Wizara ya Mambo ya Kigeni ilisema katika taarifa kwenye jukwaa la X, na "tunathibitisha kupinga ghasia".

Mkazi wa Magdeburg Dorin Steffen aliiambia DPA kwamba alikuwa kwenye tamasha katika kanisa la jirani wakati aliposikia ving'ora. Anasema vilikuwa vinatoa sauti kubwa "Ni lazima uhisi kwamba kuna jambo baya limetokea."


Ujerumani inaomboleza shambulizi la Berlin

Aliita shambulizi hilo "siku ya giza" kwenye jiji hilo. "Tunatetemeka," Steffen alisema. "Ninawahurumia jamaa, lakini pia ninatumaini kwamba hakuna kilichowapata jamaa zetu, na marafiki zetu."

Baada ya mechi ya soka Ijumaa jioni kati ya Bayern Munich na Leipzig, Mkurugenzi Mtendaji wa Bayern Jan-Christian Dreesen aliwaomba mashabiki wa klabu hiyo kukaa kwa ukimya kwa dakika moja kufuatia shambulizi hilo.