1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tshisekedi amrejesha Jean-Pierre Bemba serikalini

24 Machi 2023

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi amemteua makamu wa zamani wa rais Jean Pierre Bemba kuwa waziri wa ulinzi.

https://p.dw.com/p/4P9l9
Jean-Pierre Bemba
Picha: picture-alliance/AP Photo/M. Kooren

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi amefanya uteuzi huo katikati ya mabadiliko makubwa baraza la mawaziri.

Pierre Bemba kiongozi wa zamani wa wanamgambo aliyehukumiwa kifungo cha miaka 10 na mahakama ya kimataifa ya makosa ya uhalifu, ICC kwa madai ya uhalifu wa kivita anakuwa miongoni mwa wateule wengine katika baraza lenye mawaziri 57.

Msemaji wa serikali amesema uteuzi wake ulikuwa ni wa muhimu na wa dharura, katika tangazo alilolitoa kupitia televisheni ya taifa jana usiku. Bemba alikuwa makamu wa rais kati ya mwaka 2003 hadi 2006.

Mabadiliko haya ya mawaziri ambayo ni makubwa zaidi ya wafuatiliaji walivyobashiri, yanafanyika kabla ya uchaguzi wa rais unaotarajiwa Disemba 20 ambao Tshisekedi huenda akawania awamu ya pili.

Soma zaidi: Bemba arejea tena DRC

Taifa hilo kwa sasa liko katika vita dhidi ya makundi ya wanamgambo na hususan la M23 linalofanya uasi na ambalo Kinshasa na mataifa ya magharibi wanasema linaungwa mkono na Rwanda.