1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTaiwan

Tsai: Amani ni suluhisho kati ya Taiwan na China

10 Oktoba 2023

Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen amesema amani kati ya Taiwan na China ndilo chaguo pekee kusuluhisha tofauti za kisiasa.

https://p.dw.com/p/4XLHh
Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen
Rais wa Taiwan Tsai Ing-wenPicha: Chiang Ying-ying/AP/dpa/picture alliance

Amesisitiza umuhimu wa kisiwa hicho chenye utawala wake wa ndani, kujilinda dhidi ya vitisho vya China kutaka kukivamia.

Katika hotuba aliyoitoa wakati wa sikukuu ya kitaifa hivi leo rais Tsai amesema jumuiya ya kimataifa inauona utulivu na uthabiti wa eneo la mlango bahari wa Taiwan kama kipengee muhimu kwa usalama na ustawi wa dunia.

China inakichukulia kisiwa cha Taiwan kama himaya yake na imekuwa ikipeleka meli na madege ya kivita katika mlango bahari wa Taiwan katika juhudi ya kuwatisha wakazi milioni 23 ambao wengi wanaounga mkono kuendelea kuwa na uhuru wao wa ndani.