1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump: Nipo tayari kwa mdahalo na Harris Septemba 4

3 Agosti 2024

Mgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Republican Donald Trump amesema kuwa amekubaliana na kituo cha televisheni cha Fox News kufanya mdahalo mnamo Septemba 4 na mgombea wa cham cha Democratic Kamala Harris.

https://p.dw.com/p/4j4l4
 Donald Trump na Kamala Harris
Mgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Republican Donald Trump amesema kuwa amekubaliana na kituo cha televisheni cha Fox News kufanya mdahalo mnamo Septemba 4 na mgombea wa chama cha Democratic Kamala Harris

Mgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Republican Donald Trump amesema kuwa amekubaliana na kituo cha televisheni cha Fox News kufanya mdahalo mnamo Septemba 4 na mgombea wa cham cha Democratic Kamala Harris.

Akitumia mtandao wake wa Truth Social, Donald Trump amesema amekubali kuwa na mdahalo na Kamala Harris ingawa bado haijafahamika iwapo makamu huyo wa rais ataridhia kushiriki.

Hatua hiyo ya Trump inajiri saa chache baada ya Harris kupata uteuzi wa chama chake cha Democratic wa kugombea Urais katika uchaguzi wa hapo mwezi Novemba.

Jitihada za Trump kurejea katika Ikulu ya White House zilipinduliwa mnamo Julai 21 wakati Rais Biden aliyekuwa anakabiliwa na wasiwasi juu ya umri wake alipojiondoa katika kinyanganyiro hicho na kumuacha kijiti makamu wake Kamala Harris.