1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump mahakamani ili kujitetea kuwa na kinga ya kutoshtakiwa

9 Januari 2024

Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trum, amefika katika mahakama ya shirikisho mjini Washington katika kesi ya kusikiliza hoja yake mpya ya kujitetea kwamba, kama rais wa zamani ana kinga.

https://p.dw.com/p/4b1sl
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump
Rais wa zamani wa Marekani Donald TrumpPicha: Louis Lanzano/UPI Photo/IMAGO

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani, hukumu ya kesi hiyo inatarajiwa kutolewa Machi 4 mwaka huu mjini Washington katika mahakama iliyoko karibu na jengo la Bunge lililovamiwa na wafuasi wa kiongozi huyo wa zamani wa Marekani mnamo Januari 6, 2021.

Mawakili wa Trump wanajaribu kuyazima mashtaka dhidi ya mteja wao kwa kutowa hoja mpya, kwamba rais huyo wa zamani ana "kinga kamili" na hawezi kufunguliwa mashtaka yeyote kutokana na hatua zake alizochukuwa akiwa bado katika Ikulu ya White House.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW