Trump aiandaa Guantanamo kuwa kituo cha wahamiaji 30,000
30 Januari 2025Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza mipango ya kuandaa kituo cha kuzuwilia wakimbizi katika gereza la kijeshi la Guantanamo, kwa ajili ya hadi wakimbizi 30,000.
Kituo hicho, ambacho ni tofauti na gereza lenye ulinzi mkali, kimetumika hapo awali kuhifadhi wakimbizi, wakiwemo Wahaiti na Wacuba waliokamatwa baharini. Hatua hii ni sehemu ya juhudi za Trump kudhibiti uhamiaji haramu.
Soma pia: Trump asaini maagizo kadhaa ya rais
Rais wa Cuba, Miguel Diaz-Canel, ameielezea mipango hiyo kuwa ya ukatili, akidai kuwa wakimbizi hao watawekwa karibu na vituo vilivyotumika kwa mateso na vifungo vinavyokiuka sheria.
Wakati huo huo, vyama vya wafanyakazi wa serikali vimewashauri wanachama wake kuwa makini na pendekezo la Trump la "mpango wa kujitolea kujiuzulu," utakaowawezesha wafanyakazi kujiuzulu kwa malipo ya mshahara wa miezi minane.