1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa ulinzi wa Marekani Mark Esper afutwa kazi

10 Novemba 2020

Viongozi katika utawala wa rais Donald Trump umepuzilia mbali matokeo ya uchaguzi, huku Trump akiwazuia maafisa wa serikali kutoshirikiana na rais mteule Joe Biden

https://p.dw.com/p/3l5dx
US Wahl 2020 Donald Trump
Picha: Tom Brenner/REUTERS

Baadhi ya wanachama wa Republican, pamoja na kiongozi wa wengi katika baraza la Seneti Mitch McConnell, wameunga mkono juhudi za Trump kupinga matokeo ya uchaguzi na ni wachache pekee waounga mkono ushindi wa Biden, na kulaani hatua ya Trump kumfuta kazi waziri wa Ulinzi Mark Esper.

Muendelezo wa matukio hayo unatia shaka iwapo taifa hilo litashuhudia mabadiliko ya uongozi kwa mustakabali wa amani na utaratibu kama ilivyokuwa katika miaka iliyopita hatua ambayo imekita mizizi katika kuimarisha Demokrasia yake ya muda mrefu. soma zaidi Joe Biden bado anahitaji uvumilivu 

Mfumo wa wajumbe wa uchaguzi umeratibiwa kutoa matokeo rasmi ya ushindi wa Biden mnamo Desemba 14 na mwanademokrasia huyo ataapishwa kuingia ofisini mwishoni mwa Januari 20, 2021.

Mwanasheria mkuu William Barr ameagiza uchuguzi

USA Protest nach dem Tod von George Floyd | Trump und Barr
Mwanasheria mkuu William Barr na rais Donald Trump katika ikulu ya White HousePicha: picture-alliance/CNP/AdMedia/D. Mills

Hapo jana, Barr aliidhinisha mawakili kufanya uchunguzi kuhusu madai ya wizi wa kura na ulaghai katika uchaguzi, ingawa hapana visa vyovyote vilivyoripotiwa kuhusu tatizo hilo katika uchaguzi wa 2020.

Maafisa wa uchaguzi kutoka vyama vyote vya kisiasa pamoja na waangalizi wa kimatifa wamesema  upigaji kura ulikwenda vizuri na hakukuwa na kasoro.

Biden tayari ameanza mipango ya kujenga utawala wake, na kuandaa timu ya wataalam kukabili janga linalozidi kuongezeka la Corona, Lakini wanaopaswa kutoa mwelekeo wa kuanza rasmi kwa zoezi hilo wamekwama kutokana amri ya rais Trump. Huku rais Trump akiendelea kuwachukulia hatua wanaokaidi amri yake.

Seneta Chuck Schumer wa Republican amesema hatua ya Republican kukataa kukubali matokeo ya uchaguzi ni hatari sana na ni sumu kali kwa demokrasia ya Marekani.

Republican wamekuwa wakisita kumshinikiza Trump kwenda kukubali ushindi wa Biden, wakijua ingemkasirisha na kuvuruga msingi wa uhusiano wao wa Trump.

Wengi pia hawakuwa wakimuhimiza Trump kuhusu madai ya kuwepo udanganyifu katika uchaguzi kwa wakiashiria kuwa madai hayo hayakuwa na msingi.

Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Utawala katika ikulu ya Marekani Emily murphy aliyeteuliwa na Trump hajaanza mchakato wa kuelekeza utawala mpya wala hajatoa muongozo ni lini ataanza mchakato huo.

Ukosefu huo wa ufafanuzi unachochea maswali ikiwa Trump anatumia muda wake mwingi uliobaki ofisini kumzuia Biden kuunda serikali yake. Biden hadi sasa kwa kiasi kikubwa amekuwa akimpuuza Trump na badala yake kumuomba washirikiane.

Biden azidi kupongezwa kwa ushindi licha ya Trump kukataa kukubali kushindwa