1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump asubiri kuthibitishwa kuwa mgombea wa Republican

15 Julai 2024

Chama cha Republican leo Jumatatu, kinaanza mkutano wake mkuu, utakaomtambulisha rasmi Donald Trump kama mgombea wa chama hicho katika uchaguzi wa rais wa Novemba 5 nchini Marekani.

https://p.dw.com/p/4iIY1
Mkutano mkuu wa chama cha Republican unafanyika kwenye mji wa Milwaukee
Mkutano mkuu wa chama cha Republican unafanyika kwenye mji wa Milwaukee.Picha: Ines Pohl/DW

Mkutano huo unafunguliwa siku chache baada ya jaribio la kumuua rais huyo wa zamani.  Trump anatarajiwa kuidhinishwa na wajumbe wengi kupeperusha bendera ya chama chake  lakini pia anatarajiwa kutangaza mgombea mwenza.

Mkutano huo wa Republican wa siku nne utafanyika katika mji wa Milwaukee katika jimbo la Wisconsin.

Siku mbili zilizopita Trump alinusurika kuuwawa kwa kupigwa risasi katika mkutano wake wa kampeni,katika tukio lililosababisha mshtuko mkubwa ndani na nje ya Marekani.

Trump na watu wengine wawili walijeruhiwa huku mtu mmoja akiuwawa.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW