Trump asaini amri ya mageuzi ya polisi
17 Juni 2020Matangazo
Rais Trump amesema mageuzi hayo yanalenga kuleta haki. Amri hiyo ya rais inatoa ufadhili kwa idara ya polisi kote nchini humo, na inapiga marufuku mbinu ya polisi kumkabili mshukiwa kwa njia inayomfanya asiweze kupumua kama hatua ya kumdhibiti, ila tu ikiwa maisha ya polisi yako hatarini.
Amri hiyo pia inahimiza mafunzo zaidi kuhusu miongozo ya kutumia nguvu, na pia ukusanyaji wa taarifa au data za polisi ambao wamejihusisha na mienendo mibaya.
Trump amesema wanapaswa kuachana na mbinu za zamani ambazo zimefeli, na kwamba kinachohitajika sasa si hofu na migawanyiko, bali kuimarisha uzingatifu wa sheria na kuzileta jamii pamoja.