1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump apigwa faini kwa kesi isiyo na msingi

20 Januari 2023

Jaji John Middlebrooks wa mahakama ya shirikisho nchini Marekani amewapiga faini ya kiasi dola milioni moja rais wa zamani Donald Trump na mawakili wake kwa kufungua kile alichokiita kesi isiyokuwa na maana.

https://p.dw.com/p/4MTTZ
Trump For President 2024: It's Official
Picha: Al Diaz/Miami Herald/ZUMA/picture alliance

Kulingana na Jaji John Middlebrooks wa mahakama hiyo, kesi hiyo ilikuwa na madai kwamba Hillary Clinton alijaribu kufanya udanganyifu katika uchaguzi wa mwaka 2016. Jaji  Middlebrooks amesema Mrepublican huyo anayetaka  kurudi madarakani mwaka 2024 ameonesha kile alichokiita mtindo wa kuendelea kuzitumia vibaya mahakama na alifungua kesi kutumia uwongo kuendeleza mtazamo wake wa  kisiasa. Katika kesi hiyo mwaka jana Trump alidai Clinton aliyeshindwa uchaguzi wa rais mwaka 2016 alianzisha taarifa za uwongo kwamba kampeini yake ilishirikiana na Urusi na kwa hivyo Trump alitaka kulipwa dola milioni 70 kwa kuchafuliwa jina. Jaji Middlebrooks amesema kesi hiyo haikupaswa kufikishwa mahakamani.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW