1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump apatikana na hatia katika kesi ya uhalifu

31 Mei 2024

Kundi la kampeni za uchaguzi la Rais wa Marekani Joe Biden, limesema uamuzi uliomtia hatiani rais wa zamani wa nchi hiyo Donald Trump kwa mashtaka ya jinai, umethibitisha kuwa hakuna aliye mkuu kuliko sheria

https://p.dw.com/p/4gTMv
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akihutubia waandishi habari alipokuwa akitoka mahakamani mnamo Mei 30, 2024
Rais wa zamani wa Marekani Donald TrumpPicha: Justin Lane/EPA

Baada ya uamuzi huo, msemaji wa kampeini ya Biden Michael Tyler, alisema bado kuna njia moja ya kumzuia Trump kutorejea madarakani ambayo ni kupitia kura.

Trump ni rais wa kwanza wa Marekani kupatikana na hatia ya uhalifu

Hapo jana, Trump alikuwa rais wa kwanza wa Marekani kupatikana na hatia ya uhalifu baada ya jopo moja la New York kumtia hatiani kwa kughushi rekodi za biashara ili kuficha kashfa ya ngono wakati wa kampeni za mwaka 2016.

Kupatikana na hatia kwa Trump huenda kukaathiri uchaguzi wake

Kura za maoni zinaonyesha kuwa kupatikana na hatia kwa Trump huenda kukamsababishia hatari katika uchaguzi ambao unaweza kuamuliwa tu kwa makumi ya maelfu ya kura katika majimbo machache.

Lakini baadhi ya wataalamu wanasema tishio hilo huenda lisiwe kubwa.