1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump amshinda Haley katika jimbo la South Carolina

Sylvia Mwehozi
25 Februari 2024

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ameshinda kura za mchujo na kumbwaga mpinzani wake Nikki Haley katika jimbo lake la nyumbani la South Carolina.

https://p.dw.com/p/4crA3
 Donald Trump | South Carolina
Donald Trump huko South CarolinaPicha: Andrew Harnik/AP Photo/picture alliance

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ameshinda kura za mchujo na kumbwaga mpinzani wake Nikki Haley katika jimbo lake la nyumbani la South Carolina katika kinyang'anyiro cha kuwania uteuzi wa mgombea urais wa chama cha Republican.

Soma pia: Trump aanza vyema safari yake ya kuwania urais Marekani

Trump amekuwa akipewa nafasi kubwa ya kushinda katika jimbo hilo la kusini licha ya kukabiliwa na orodha ndefu ya mashitaka ya jinai na hadhi ya Haley kama mzaliwa wa jimboni humo aliyewahi kushinda mihula miwili kama gavana.

Ushindi huo mkubwaumezidisha miito kutoka kwa washirika wa Trump wanaomtaka Haley ambaye ni mpinzani pekee aliyesalia kujiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho.

Lakini mwanamama huyo amesisitiza kwamba ataendelea kupambana na Trump hadi mnamo Machi 5 wakati Warepublican kwenye majimbo 15 watakapopiga kura kumteua mgombea wa urais.