1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMarekani

Trump akutwa na hatia ya unyanyasaji wa kingono

10 Mei 2023

Baraza la wazee wa mahakama ya mjini New York limemkuta rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na hatia ya kumnyanyasa kingono na kumchafulia jina mwandishi wa habari E. Jean Carroll.

https://p.dw.com/p/4R8eM
Mwandishi wa habari E. Jean Carroll aliyemfungulia kesi ya unayanyasaji wa kingono rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, ambaye amekutwa na hatia ya unyanyasaji.
Kumekuweko na visa vingi vya uyanyasaji wa kingono dhidi ya wanawake kote ulimwenguni, lakini vingi havizungumzwi hadharani.Picha: Seth Wenig/AP/picture alliance

Kufuatia hatua hiyo, rais huyo wa zamani Donald Trump ameagizwa kulipa dola milioni tano kama fidia na faini katika kesi hiyo. Hata hivyo, jopo hilo la wazee wa mahakama limepinga madai ya Carroll kuwa Trump alimshambulia kingono katika mwaka wa 1996. Carroll alitoa ushahidi kwamba Trump alimnyanyasa kingono katika chumba cha kujipima nguo katika duka la kifahari kwenye mtaa wa Manhattan. Alisema Trump kisha alimchafulia jina lake kwa kuandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social mwaka wa 2022 kwamba madai yake yalikuwa ya uwongo. Trump anasititiza kuwa hakumnyanyasa Carroll au hata kumfahamu. Hakuhudhuria kesi hiyo. Ameuelezea uamuzi huo kuwa ni fedheha. Trump analenga kugombea uchaguzi wa rais mwaka wa 2024