1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TRIPOLI: Wakaguzi wa silaha waridhishwa na Libya

30 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFnp

Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la ukaguzi wa zana za atomiki, Mohamed El BARADEI, ameipongeza Libya kwa ushirikiano wake na wachunguzi wa taasisi hiyo waliotembelea vituo 4 vya nchi hiyo vya nishati ya nuklia. Bwana El BARADEI alitoa matamshi hayo wakati wa mazungumzo yake mjini Tripoli na kiongozi wa Libya Kanali Muamar GADDAFI baada ya ziara hiyo ambayo ni ya kwanza kuwahi kufanywa na wakaguzi hao wa kimataifa katika mitambo ya nuklia ya Libya. Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa alisema pia kuwa Libya imemkubalia kusaini kifungu cha ziyada cha mkataba wa kimataifa wenye kupiga marufuku usambazaji wa silaha za nuklia na kuahidi kuruhusu uchunguzi zaidi wa wakaguzi wa zana hizo. Kanali Muamar GADDAFI ametumia nafasi hiyo kumthibitishia El BARADEI kuwa Libya imeamua kuachana kabisa na mpango wake wa kuunda zana zilizopigwa marufuku kimataifa.