1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TRIPOLI: Wakaguzi wa silaha kuwasili Libya

28 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFoR

Mkuu wa Shirika la kimataifa la Ukaguzi wa Silaha Mohamed El BARADEI amewasili mjini Tripoli akiongoza ujumbe wa wataalamu wa mambo ya silaha kwa mazungumzo zaidi na viongozi wa Libya kuhusu miradi ya kinulia ya nchi hiyo. Ziara hiyo ni ya kwanza nchini Libya ya wakaguzi wa silaha wa Shirika hilo la Umoja wa Mataifa tangu serikali ya Tripoli ilipotangaza wiki iliopita hatua ya kukomesha mpango wake wa kuunda silaha zisizoruhusiwa kimataifa. Akiongea na wandishi wa habari baada ya kuwasili mjini Tripoli, El BARADEI alisema hakuna ushahidi unaobainisha hadi sasa kuwa Libya ilikuwa karibu kuunda silaha za nuklia. Kiongozi huyo wa Shirika la Umoja wa Mataifa la ukaguzi wa silaha ametaja kuwa ujumbe wake ni kupata ufafanuzi zaidi kuhusu mpango mzima wa Libya wa silaha za nuklia.