1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TRIPOLI: Wakaguzi wa silaha kuipekua Libya

29 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFoG

Wakaguzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Nishati ya Atomiki, wanaozuru Libya tangu mwishoni mwa wiki, wametembelea na kupekua vituo 4 vya nchi hiyo vya nishati ya nuklia. Uchunguzi huo ni wa kwanza kufanyika Libya tangu serikali ya Tripoli itangaze hivi majuzi nia ya kuachana na miradi ya kuunda silaha zisizoruhusiwa kimataifa. Wakaguzi hao wanaongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo la Nishati ya Atomiki, Mohammed el BARADEI, ambae leo anatarajiwa kukutana kwa mazungumzo na Waziri Mkuu wa Libya pamoja na mkuu wa idara ya utafiti wa nuklia.