1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TRIPOLI: Wakaguzi wa silaha kuikagua Libya

22 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFqV

Afisa mmoja wa ubalozi wa nchi ya Magharibi mjini Tripoli amekaririwa na shirika la habari la Reuters akithibitisha kuwa Libya imeamua kutoa kibali kwa wakaguzi wa kimataifa wa silaha za nuklia kuipekua mitambo yake ya nishati. Mwanadiplomasia huyo ametaja kuwa maafisa wa Libya wametoa kauli hiyo baada ya majadiliano na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki, Mohammed El BARADEI. Taarifa hiyo imetolewa siku 2 baada ya serikali ya Tripoli kutangaza nia ya kuachana na mpango wa kuunda bomu la nuklia na aina nyengine ya silaha za maangamizi. Libya iliondolewa vikwazo vya kimataifa mapema mwaka huu baada ya kukubali kubeba dhamana ya mlipuko wa ndege ya Marekani iliyoanguka juu ya anga ya Lockerbie nchini Scotland miaka 15 iliopita ambapo watu 270 walifariki dunia.