Tokyo. Tamasha la muziki kuhusu Afrika laanza huko Tokyo.
2 Julai 2005Tamasha la kwanza kati ya matamasha kadha ya muziki yenye lengo la kutoa mbinyo kwa wanasiasa kuweza kujitahidi zaidi kupambana na umasikini katika bara la Afrika limeanza katika mji mkuu wa Japan , Tokyo. Matamasha hayo manane yanayohusisha wanamuziki maarufu wa kimataifa yanafanyika katika miji 10 duniani kote.
Yanafanyika siku chache tu kabla ya mkutano wa viongozi wa kundi la G8 la mataifa yenye utajiri wa viwanda nchini Scotland.
Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair ameliweka suala la kupambana na umasikini katika bara la Afrika katika agenda ya juu kabisa katika mkutano huo wa G8.
Mwanamuzi wa Ireland Bob Geldof ndie aliyetayarisha matamasha hayo manane. Na ndie aliyetayarisha tamasha la kuisaidia Ethiopia miaka 20 iliyopita. Tamasha litakalofanyika nchini Ujerumani katika mji mkuu wa Berlin linatarajiwa kuanza saa chache zijazo.