Tokyo. Polisi waanza uchunguzi wa ajali ya treni nchini Japan.
26 Aprili 2005Matangazo
Polisi nchini Japan wamevamia ofisi za waendeshaji wa shirika la reli mjini humo la JR West wakitafuta ushahidi kuhusiana na ajali ya treni iliyotokea jana. Watu sabini na tatu wameuwawa na zaidi ya 400 wengine wamejeruhiwa wakati treni ya mjini ilipojigonga katika nyumba baada ya kutoka katika reli katika mji wa Amagasaki. Mji huo uko kiasi cha kilometa 400 kutoka mji mkuu Tokyo. Wachunguzi wanaoangalia sababu za ajali hiyo wamesema kuwa waangalia sehemu mbali mbali za uwezekano wa sababu hizo.