TOKYO. Japan yaahidiwa na umoja wa Ulaya kwamba China haitauziwa silaha.
15 Aprili 2005Matangazo
Mjumbe wa jumuiya ya Ulaya ameiahidi Japan leo kwamba jumuiya hiyo itaizingatia hatua ya serikali ya Tokyo kupinga China kuuziwa silaha. Ahadi hiyo imetolewa wakati hali ya wasiwasi kati ya mataifa hayo ya Asia ikiendelea kuongezeka na kukiwa na dalili kwamba umoja wa Ulaya utaendelea kushikilia msimamo wake wa kutoiuzia silaha China. Annalisa Giannella amekutana na wabunge wa Japan waliolezea wasiwasi wao kuhusu China kuuziwa silaha. Serikali ya Tokyo na Marekani zinasema kuiuzia silaha China kutatoa ujumbe mbaya juu ya haki za binadamu na huenda kukauzorotesha utawala, kufuatia hatua ya Beijing kupitisha sheria inayoruhusu matumizi ya nguvu iwapo Taiwan itataka kuwa huru rasmi.