Rais mteule wa Nigeria ataka ushirikiano na upinzani
2 Machi 2023Rais mteule wa Nigeria Bola Tinubu ametoa wito kwa wapinzani wake na wafuasi wao kuungana naye, baada ya uchaguzi uiliokuwa na ushindani mkali ambao vyama vya upinzani vinatafuta namna ya kuupinga kwa kudai uligubikwa na vitendo vya udanganyifu.
Tinubu mwenye umri wa miaka 70, gavana wa zamani wa jiji la Lagos, alitangazwa mshindi baada ya uchaguzi wa Jumamosi, na kutimiza ndoto yake ya muda mrefu ya kuliongoza taifa hilo lenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika. Wakati mtangulizi wake Rais Muhammadu Bihari anajiweka kando mwezi Mei, ikiwa ni baada ya kuliongoza taifa hilo kwa mihula miwili, raia wengi wa Nigeria wana imani kuwa kura zao zitampa kiongozi mpya uwezo wa kukabliana na kuzorota kwa hali ya usalama, kuinua hali ya uchumi na kupunguza umasikini.
Tinubu ataka taifa kuungana kuijenga nchi
Katika hafla maalumu ya jana Jumatano ya kukabidhiwa cheti cha ushindi wake iliyoandaliwa na Tume ya Uchaguzi, Tinubu aliwataka wapinzani kuja pamoja ili waanze ujenzi mpya wa taifa."Najua wengi hawakunipigia kura, na mmesikitishwa kuwa mgombea wenu hayupo hapa nilipoposimama sasa. Ninaelewa uchungu wako, hasira yako, tamaa. Natoa faraja kutoka kwa mwanafamilia mmmoja hadi mwingine. Lakini huu mradi mkubwa uitwao Nigeria unatuhitaji sote. Ni mkubwa na muhimu zaidi kuliko mgawanyiko wowote wa kichama." alisema Mteule Tinubu.
Katika hotuba yake hiyo Tinubu kasikia akitoa kauli za faraja kwa Wanaijeria kwa kusema ni wakati wa kufanya palipo na vitendo vya kinyama, watabadilisha kuwa mahali pa udugu. Pale kwe ghasia watastawisha amani, sehemu ya chuki kufanywa kuwa mahala pa upendo.
Pongezi kutoka kwa Marekani na Uingereza
Nje ya Nigeria Waziri Mkuu wa Uingereza ameupongea ushindi wa Tinubu kwa kusema uhusiano wa Nigeria na taifa lake bado imara na kwamba natarajia kufanya kazi pamoja na mteule katika nyanja ya usalama, kpanua wigo wa fursa za kibiashara na kustawisha maslahi ya mataifa yote mwaili.
Marekani nayo imetoa pongezi kama hizo ikisema inawapongeza watu wa Nigeria, rais mteule Tinubu na viongozi wote wa kisiasa.
Soma zaidi:Maoni: Uchaguzi wa Nigeria na mwanga wa matumaini
Matokeo ya mwisho yalimpa Tinubu wa chama tawala cha All Progressives Congress (APC), kura milioni 8.8, huku wagombea wakuu wa upinzani Atiku Abubakar na Peter Obi wakiambulia milioni 6.9 na mwingine milioni 6.1.
Vyanzo: AP/AFP/RTR