1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tinubu aongoza awali katika matokeo ya Nigeria

28 Februari 2023

Mgombea wa Urais wa chama tawala nchini Nigeria, Bola Tinubu anaongoza kwa kura katika majimbo 20 kati ya 36 nchini Nigeria.

https://p.dw.com/p/4O3BD
Nigeria Wahlen 2023/Präsidentschaftskandidat Bola Ahmed Tinubu
Picha: Emmanuel Osodi/AP Photo/picture alliance

Matokeo hayo ya awali ni kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliokusanywa na shirika la habari la la Uingereza Reuters. Lakini wapinzani wamelisusia zoezi la kuhesabu kura kwa kuonesha mashaka ya vitendo vya udanganyifu.

Matokeo ya awali kwa majumuisho kwa ngazi ya majimbo kutoka kwa tume ya uchaguzi yanaonesha Tinubu wa chama tawala cha All Progressives Congress (APC) yuko mbele kwa kura aslimia 39.7 sawa na milioni 5.4, dhidi ya Atiku Abubakar wa chama kikuu cha upinzani cha People's Democratic Party (PDP) akiwa na kiasi cha kura milioni 4.4.sawa na asilimia 32.2.

Peter Obi kipenzi cha kizazi kipya Nigeria

Nigeria vor Präsidentschaftswahl Lagos | Kandidat Peter Obi
Mgombea urais wa Nigeria Peter ObiPicha: Sunday Alamba/AP/picture alliance

Mgombea ambae anaonekana kama katokea nje kabisa katika wigo wa siasa wa Nigeria Peter Obi wa chama kidogo cha Labour anashika nafasi ya tatu kwa kura milioni 2.2 ikiwa sawa na asilimia 16.3

Takriban zaidi ya thuluthi mbili ya idadi jumla ya kura kwa taifa hilo lenye idadi kubwa zaidi ya watu bado haijatangazwa. Lakini ushindi katika jimbo la Lagos - kwa kura 582,454 dhidi ya 572,606 kwa Tinubu imekuwa hatua kubwa kwa kwa Obi, ambe ameonesha kwa wagombea kutoka kambi mbili za muda mrefu ambazo zimkuwa zikipishana katika kuongoza taifa hilo tangu kumalizika kwa utawala wa jeshi mwaka 1999.

Vitendea kazi duni katika maeneo mengi ya uchaguzi

Uchaguzi umekuwa ukikabiliwa na matatizo ya vitendea kazi na teknolojia, mambo ambayo yamesababisha kushindwa kutolewa matokeo katika maeneo mengi. Katika maeneo mengi kupakua matokeo moja kwa moja kwa njia ya mtandao kama ilivyoahidiwa na tume ya uchaguzi ya Nigeria limekuwa tatizo.

Hakujawa na shuruti ya kisheria yenye kuilazimisha tume katika kuwajibika kwa namna hiyo lakini kushindwa kwake kunamaanisha matokeo lazima yajumlishwe kwa njia ya kawaida katika kituo cha kupigia kura pamoja na eneo la kukusanyia matokeo hayo yaliopangwa na serikali.

Kwa upande wa upinzani umeendelea kuwaa katika hali ya kutoridhishwa na matokeo hayo. Mgombea Obi amesema mchakato wa uchaguzi umevurugwa, na kwamba kutokana na hali hiyo wanajitenga na kile kinachowasilishwa kwa umma juuu ya matokeo hayo.

Meneja wa kampeni ya Atiku wa chama cha PDP, Melaye Dino akiwa katika kituo cha kujumlisha matokeo cha Abuja amesema wamepotezaa matumani na matokeo hayo. Akin Oshintokun, mkurugenzi wa kampeni katika timu ya kampeni ya Obi ametoa wito wa tume ya uchaguzi wa Nigeria kuzingatia muongozo wake lakini kinyume chake waache kutangaza matokeo.

Soma zaidi:Chama cha upinzani chapata kura nyingi katika jimbo la Lagos,Nigeria

Uchaguzi wa Nigeria kwa kiwango kikubwa unategemea teknolojia ya mawasiliano, ambayo kwa sehemu kubwa imeonekana kutozaa matundaa yoyote, na kutokuwepo na njia za wazi yaa kuyapinga matokeo kisheria. Obi alimshinda mpinzani wake wa chama tawala kwa kushinda katika kitovu cha kibiashara cha jiji la Lagos kukiwa ghasia kubwa na ucheleweshaji na malalamiko ya ukiukwaji wa taratibu.

Vyanzo: RTR/AFP