1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Thomas-Greenfield akutana na wakimbizi wa Sudan nchini Chad

Josephat Charo
7 Septemba 2023

Mjumbe wa Marekani aktika Umoja wa Mataifa amekutana na wakimbizi wa Sudan nchini Chad waliokimbia hali ya vita na machafuko nchini mwao.

https://p.dw.com/p/4W2Rl
US-Botschafterin bei der UN Linda Thomas-Greenfield
Picha: DAVID DEE DELGADO/REUTERS

Mjumbe maalumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield, amekutana na wakimbizi wa Sudan nchini Chad wanaokimbia machafuko ya kikabila na hujuma za ngono kutokana na vita. Akiwa katika ziara ya mji wa Adre katika mpaka wa Sudan na Chad,

Thomas-Greenfield alikutana na wanawake saba wa Sudan waliomuelezea jinsi walivyoyakimbia machafuko nchini mwao. Mjumbe huyo wa Marekani amesema wanawake hao walikimbilia Chad kutokana na hofu na hakuna aliyeonyesha nia ya kutaka kurejea nyumbani wakati machafuko yakiendelea.

Wakati haya yakiarifiwa, raia wapatao 32 wameuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mashambulizi ya makombora yaliyofanywa na jeshi la Sudan siku ya Jumanne. Taarifa iliyotolewa jana imesema mashambulizi hayo yamefanywa katika kitongoji cha Ombada magharibi mwa mji wa Omdurman ambacho kimeshuhudia mashambulizi kadhaa ya umwagaji damu.