1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

THE HAGUE : Watu 7 mbaroni kwa ugaidi

14 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CERx

Polisi ya Uholanzi imewakamata watu saba katika misako ya kupiga vita ugaidi leo hii kwa tuhuma za kupanga mashambulizi dhidi ya wanasiasa na majengo ya serikali.

Wakati wa misako hiyo milio ya risasi ilisikika mjini The Hague ambayo ni makao makuu ya serikali ya Uholanzi na kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchi hiyo haikuweza kufahamika mara moja nani aliyefyetuwa risasi hizo au iwapo kuna mtu yoyote yule aliyejeruhiwa.

Mratibu wa taifa wa kupiga vita ugaidi Tjibbe Joustra amesema watu wanaotuhimiwa kujishughulisha na harakati za uagidi wamekamatwa na polisi imeimarisha usalama katika majengo kadhaa ya serikali zikiwemo ofisi za Waziri Mkuu Jan Peter Balkenede mjini The Hague.