1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

The Hague. Waholanzi nao kuikataa katiba ya Ulaya katika kura ya maoni.

21 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFBn

Kura ya maoni iliyofanywa na kituo kimoja cha televisheni nchini Uholanzi inaonesha kuwa wengi wa wapiga kura nchini humo wataikataa katiba ya Ulaya katika kura ya maoni itakayofanyika hapo Juni mosi.

Kura hiyo ya maoni iliyoendeshwa na kituo hicho cha Televisheni inaonesha matokeo ya juu juu tu, lakini wanasiasa wamesema kuwa wanayachukulia matokeo hayo kwa dhati. Kura ya maoni ya hapo Juni itafanyika siku tatu tu baada ya kura kama hiyo kufanyika nchini Ufaransa, ambako kambi itakayopiga kura ya hapana pia inaonesha kupata ushindi.