1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

THE HAGUE: Uhalifu uliotendewa Darfur unachungzwa rasmi

7 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF6A

Mahakama ya Kimataifa mjini The Hague-Uholanzi,inayoshughulika na uhalifu vitani, imeanzisha uchunguzi rasmi kuhusu tuhuma kuwa kumefanyika uhalifu katika vita vya Darfur magharibi mwa Sudan.Serikali ya Sudan lakini imesema haijafurahishwa na uchunguzi wa aina hiyo.Mahakama ya Kimataifa imepokea kutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa orodha ya majina ya watu wanaoshukiwa kuhusika na mauaji na ubakaji katika jimbo la Darfur.Miongoni mwa wale waliotajwa ni maafisa wakuu wa serikali ya Sudan na viongozi wa wanamgambo.Inakadiriwa kuwa hadi watu 180,000 wameuawa katika jimbo la Darfur na zaidi ya milioni mbili wengine wamepoteza maskani zao tangu kuzuka kwa mapigano miaka miwili iliyopita.Makundi yanayopigania haki za binadamu yamekaribisha tangazo la kufunguliwa uchunguzi rasmi kwa kusema kuwa hiyo ni njia ya kuleta haki kwa wahanga wa mgogoro wa Darfur.