1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

The Hague. Mbabe wa zamani wa vita afikishwa mahakamani.

22 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG5B

Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor amefikishwa kwa mara ya kwanza katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu mjini The Hague na kufungua njia kwa ajili ya kusikilizwa kesi yake dhidi ya uhalifu wa kivita.

Mbabe huyo wa zamani wa kivita hakutoa taarifa yoyote wakati wa kikao hicho.

Taylor anakabiliwa na mashtaka 11 ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu kwa madai ya kuamuru mauaji, ubakaji na ukatwaji wa viungo kwa maelfu ya watu wakati wa vita vya wenyewe kwa wenye vilivyochukua muda wa miaka 10 nchini Sierra Leone.

Amesema kuwa hana hatia na anakabiliwa na kifungo cha maisha iwapo atapatikana na hatia.