1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

The Hague. Kesi ya wahalifu wa kivita yaanza kusikilizwa.

15 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG7W

Majaji katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita mjini The Hague wameanza kusikiliza kesi ya maafisa saba wa kijeshi wa ngazi ya juu wa Kiserb kutoka Bosnia kwa madai yanayohusika na mauaji katika mji wa Srebrenica.

Watano kati ya watuhumiwa saba wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya halaiki, pamoja na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Kiasi cha wanaume na vijana 8,000 wa Kiislamu waliuwawa na majeshi ya Waserb wa Bosnia katika mji wa mashariki ya Bosnia wa Srebrenica Julai 1995. Muda mfupi baada ya kesi hiyo kuanza , mahakama hiyo iliiahirisha kwa mapumziko ya majira ya joto. Kesi hiyo inatarajiwa kuanza kusikilizwa tena baadaye mwezi ujao.