1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Tetemeko la ardhi laua zaidi ya watu 500 Uturuki

6 Februari 2023

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.9 kwa kipimo cha Richter limepiga katikati ya Uturuki na kaskazini magharibi mwa Syria.

https://p.dw.com/p/4N8Wt
Türkei | Erdbeben Diyarbakir
Picha: IHA agency via AP/picture alliance

Na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 500, na kuharibu majengo kadhaa.Vikosi vya uokoaji vinaendelea kuwatafuta waathirika waliokwama kwenye vifusi. 

Shirika la kukabiliana na majanga la Uturukilimesema watu wengine zaidi ya 600 wamejeeruhiwa na limeomba msaada wa kimataifa katika kukabiliana na matokeo mabaya ya tetemeko hilo ambalo limefika hadi Cyprus na Lebanon.

Uturuki ni miongoni mwa nchi ambazo zimekuwa zikikumbwa na matetemeko ya ardhi mara kwa mara, ambapo mwaka 1999 watu wapatao 17,000 waliuwawa kutokana na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.6 lilipopiga mji wa Izmit na lile la 2011 katika mji wa Van lililouwa watu 500.